Picha ya Aki yazua maswali





LAGOS, NIGERIA
WIKI hii katika mitandao kadhaa ya Nigeria imesambazwa picha za mwigizaji Chinedu Ikedieze 'Aki' akiwa amemkumbatia mtoto na kuzuka habari kuwa nyota huyo wa filamu za Nigeria alipata mtoto kabla ya kuoa.

Habari zimezagaa kuwa Aki amekuwa akificha ukweli kuhusu mtoto wake ingawa taarifa za ndani zinasema kwamba mkewe aitwaye Nneoma anafahamu juu ya jambo hilo.

Hata hivyo, Aki hakutaka kutoa ufafanuzi juu ya mtoto huyo kwa madai kwamba hayo ni maisha yake binafsi.
Aki na Nneoma walifunga ndoa mwaka jana.

Mercy achekelea penzi jipya





LAGOS, NIGERIA
NYOTA wa Nollywood, Mercy Johnson amekiri kufurahia maisha kwa sasa. Dada huyo anafurahia penzi jipya la Ayo Makun maarufu kama 'Ayas'.

Rafiki wa karibu wa Mercy amesema kuwa mwanamke huyo kwa sasa anafurahia maisha ingawa haijafahamika iwapo ataishi na mwanaume huyo au la.

"Kila mara anapokuwa na mwanaume huyo huwa wanacheka tu, nadhani wamepatana sana," alisema mtu huyo.

Ayas ambaye ni mwigizaji wa filamu za vichekesho pia alimshirikisha Mercy katika filamu yake mpya iitwayo 'AY Crib'. Filamu hiyo itakuwa hewani Oktoba Mosi mwaka hu

 
Sharks Video Production © 2012 | Designed by Eddie Sucre "TUNADESIGN BLOG ZA AINA ZOTE NA ZENYE UBORA KWA BEI POA KABISA, PIA TUNAUZA DOMAIN KWA ATAYEHITAJI CALL US TODAY 0658184797, 0752184797 OR 0653522520 "