SHARK"S VIDEO PRODUCTION- Ofisi za Kam

Ofisi za kampuni

Chiki Mchoma

Gari za production

Editing

IJUE SHARK"S VIDEO PRODUCTION


Shark's Video Production ilianza rasmi Desemba 2011 ni kampuni ya kutengeneza sinema na shughuli za muziki yenye makao makuu Equator Grill Mtoni. Kampuni hii inafanya shughuli zote zinazohusiana na utengenezaji wa video, kama vile kutengenza filamu za hadithi na za documentary, kupiga picha za video za matukio kama harusi, mikutano na mikusanyiko mbalimbali, kutengeneza video za muziki na kazi kama hizo. Sharks Video Production pia inaangalia menejimenti ya kundi la wanamuziki wanaojiita  Shark Family, ambapo tayari wanamuziki wawili wa kundi hilo wamekwishatoa vibao vyao hewani. Kigwema na wimbo wake wa KWENYE MAGAZETI na SUPER ZII na wimbo wake UMECHELEWA. Kati ya filamu ambazo kampuni hii imezitengeneza  ni   Shemeji- akiwemo msanii maarufu Mshindo Jumanne
Bi Moza, Kaimu Mkurugenzi Shark's Video Production













Unknown killer-ambamo yumo msanii mwanamuziki Pacho Mwamba, na Sandra Sikitu,  Nusu ya mali yangu, Dume jeuri-ambamo tunamkuta  Chiki Mchoma ambaye wengi humkumbuka kama Ticha kwenye tamthiliya moja ya zamani ya Kaole,iliyokuwa ikirushwa na ITV. Sharks video imejidhatiti kwa kila hali kwa kuwa na vifaa bora kuanzia kamera, computer za editing na hata vifaa vya kurudufu kazi. Sharks pia inajihusisha na uagizaji na uuzaji wa vifaa 'used' vya elektroniki na ina mduka mawili moja likiwa Komakoma Mwananyama, jingine , Pile Temeke, ambako huko utapata Mafriji, mafriza, music systems, TV, DVD Players na kadhalika.

Picha ya Aki yazua maswali





LAGOS, NIGERIA
WIKI hii katika mitandao kadhaa ya Nigeria imesambazwa picha za mwigizaji Chinedu Ikedieze 'Aki' akiwa amemkumbatia mtoto na kuzuka habari kuwa nyota huyo wa filamu za Nigeria alipata mtoto kabla ya kuoa.

Habari zimezagaa kuwa Aki amekuwa akificha ukweli kuhusu mtoto wake ingawa taarifa za ndani zinasema kwamba mkewe aitwaye Nneoma anafahamu juu ya jambo hilo.

Hata hivyo, Aki hakutaka kutoa ufafanuzi juu ya mtoto huyo kwa madai kwamba hayo ni maisha yake binafsi.
Aki na Nneoma walifunga ndoa mwaka jana.

Mercy achekelea penzi jipya





LAGOS, NIGERIA
NYOTA wa Nollywood, Mercy Johnson amekiri kufurahia maisha kwa sasa. Dada huyo anafurahia penzi jipya la Ayo Makun maarufu kama 'Ayas'.

Rafiki wa karibu wa Mercy amesema kuwa mwanamke huyo kwa sasa anafurahia maisha ingawa haijafahamika iwapo ataishi na mwanaume huyo au la.

"Kila mara anapokuwa na mwanaume huyo huwa wanacheka tu, nadhani wamepatana sana," alisema mtu huyo.

Ayas ambaye ni mwigizaji wa filamu za vichekesho pia alimshirikisha Mercy katika filamu yake mpya iitwayo 'AY Crib'. Filamu hiyo itakuwa hewani Oktoba Mosi mwaka hu

 
Sharks Video Production © 2012 | Designed by Eddie Sucre "TUNADESIGN BLOG ZA AINA ZOTE NA ZENYE UBORA KWA BEI POA KABISA, PIA TUNAUZA DOMAIN KWA ATAYEHITAJI CALL US TODAY 0658184797, 0752184797 OR 0653522520 "